Je, nyinyi bado hamjui?Je, hamjapata kusikia?Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele;yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani.Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu.Maarifa yake hayachunguziki.