Isaya 35:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mchanga wa moto jangwani utakuwa bwawa la maji,ardhi kavu itabubujika vijito vya maji.Makao ya mbwamwitu yatajaa maji;nyasi zitamea na kukua kama mianzi.

8. Humo kutakuwa na barabara kuu,nayo itaitwa “Njia Takatifu.”Watu najisi hawatapitia humo,ila tu watu wake Mungu;wapumbavu hawatadiriki kuikanyaga,

9. humo hakutakuwa na simba,mnyama yeyote mkali hatapitia humo,hao hawatapatikana humo.Lakini waliokombolewa ndio watakaopita humo.

10. Waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu watarudi,watakuja Siyoni wakipiga vigelegele.Watakuwa wenye furaha ya milele,watajaliwa furaha na shangwe;huzuni na kilio vitatoweka kabisa.

Isaya 35