Isaya 34:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Nyati wataangamia pamoja nao,ndama kadhalika na mafahali.Nchi italoweshwa damu,udongo utarutubika kwa mafuta yao.

8. Maana Mwenyezi-Mungu anayo siku ya kisasi;mwaka wa kulipiza maadui wa Siyoni.

9. Vijito vya Edomu vitatiririka lami,udongo wake utakuwa madini ya kiberiti;ardhi yake itakuwa lami iwakayo.

10. Itawaka usiku na mchana bila kuzimika,moshi wake utafuka juu milele.Nchi itakuwa jangwa siku zote,hakuna atakayepitia huko milele.

11. Itakuwa makao ya kozi na nungunungu,bundi na kunguru wataishi humo.Mwenyezi-Mungu atawaletea ghasia,na timazi la fujo kwa wakuu wake.

12. Nchi itaitwa “Nchi bila Mfalme;”wakuu wake wote wametoweka.

13. Miiba itaota katika ngome zake,viwavi na michongoma mabomani mwao.Itakuwa makao ya mbwamwitu, maskani yao mbuni.

Isaya 34