Isaya 33:2-9 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Ee Mwenyezi-Mungu, utuonee huruma,kwako tumeliweka tumaini letu.Uwe kinga yetu kila siku,wokovu wetu wakati wa taabu.

3. Kwa kishindo cha sauti yako watu hukimbia;unapoinuka tu, mataifa hutawanyika.

4. Maadui zao wanakusanya mateka,wanayarukia kama panzi.

5. Mwenyezi-Mungu ametukuka,yeye anaishi juu mbinguni.Ameujaza Siyoni haki na uadilifu.

6. Enyi watu wa Yerusalemu,Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama,atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa.Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu.

7. Haya, mashujaa wao wanalia,wajumbe wa amani wanaomboleza.

8. Barabara kuu zimebaki tupu;hamna anayesafiri kupitia humo.Mikataba inavunjwa ovyo,mashahidi wanadharauliwa.Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.

9. Nchi inaomboleza na kunyauka;misitu ya Lebanoni imekauka,bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa,huko Bashani na mlimani Karmelimiti imepukutika majani yake.

Isaya 33