Isaya 33:10-14 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Sasa mimi nitainuka;sasa nitajiweka tayari;sasa mimi nitatukuzwa.

11. Mipango yenu yote ni kama makapi,na matokeo yake ni takataka tupu.Pumzi yangu itawaangamiza kama moto.

12. Watu watakuwa kama wamechomwa kuwa majivu,kama miiba iliyokatwa na kuteketezwa motoni.

13. Sikilizeni mambo mliyofanya enyi mlio mbali,nanyi mlio karibu kirini uwezo wangu.”

14. Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa,wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema:“Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali?Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”

Isaya 33