Isaya 3:9-18 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao;wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma,wala hawaifichi.Ole wao watu hao,kwani wamejiletea maangamizi wenyewe.

10. Waambieni waadilifu jinsi walivyo na bahati:Kwani watakula matunda ya matendo yao.

11. Lakini ole wao watu waovu!Mambo yatawaendea vibaya,kwani waliyotenda yatawapata wao wenyewe.

12. Watu wangu watadhulumiwa na watoto;wanawake ndio watakaowatawala.Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha,wanavuruga njia mnayopaswa kufuata.

13. Mwenyezi-Mungu yu tayari kuanza mashtaka,anasimama kuwahukumu watu wake.

14. Mwenyezi-Mungu anawashtakiwazee na wakuu wa watu wake:“Nyinyi ndio mlioliharibu shamba la mizabibu;mali walizowanyanganywa maskini zimo nyumbani kwenu.

15. Mnamaanisha nini kuwakandamiza watu wangu,kuwatendea ukatili watu maskini?Nauliza mimi Bwana, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”

16. Mwenyezi-Mungu asema:“Wanawake wa Siyoni wana kiburi;wanatembea wameinua shingo juu,wakipepesa macho yao kwa tamaa.Hatua zao ni za maringo,na miguuni njuga zinalia.

17. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitawaadhibu;nitawanyoa nywele hao wanawake wa Siyoni,na kuwavua nguo za kufunika uchi wao.”

18. Siku yaja ambapo Mwenyezi-Mungu atawanyanganya wanawake wa Yerusalemu vitu vyote wanavyoringia: Njuga, kaya, mikufu,

Isaya 3