7. Lakini siku hiyo atasema,“Mimi siwezi kuwa mwuguzi,nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi.Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”
8. Watu wa Yerusalemu wamejikwaa,watu wa Yuda wameanguka,kwa kuwa wanampinga Mwenyezi-Mungukwa maneno na matendo,wakipuuza utukufu wake miongoni mwao.
9. Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao;wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma,wala hawaifichi.Ole wao watu hao,kwani wamejiletea maangamizi wenyewe.
10. Waambieni waadilifu jinsi walivyo na bahati:Kwani watakula matunda ya matendo yao.
11. Lakini ole wao watu waovu!Mambo yatawaendea vibaya,kwani waliyotenda yatawapata wao wenyewe.
12. Watu wangu watadhulumiwa na watoto;wanawake ndio watakaowatawala.Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha,wanavuruga njia mnayopaswa kufuata.
13. Mwenyezi-Mungu yu tayari kuanza mashtaka,anasimama kuwahukumu watu wake.
14. Mwenyezi-Mungu anawashtakiwazee na wakuu wa watu wake:“Nyinyi ndio mlioliharibu shamba la mizabibu;mali walizowanyanganywa maskini zimo nyumbani kwenu.
15. Mnamaanisha nini kuwakandamiza watu wangu,kuwatendea ukatili watu maskini?Nauliza mimi Bwana, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”
16. Mwenyezi-Mungu asema:“Wanawake wa Siyoni wana kiburi;wanatembea wameinua shingo juu,wakipepesa macho yao kwa tamaa.Hatua zao ni za maringo,na miguuni njuga zinalia.
17. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitawaadhibu;nitawanyoa nywele hao wanawake wa Siyoni,na kuwavua nguo za kufunika uchi wao.”
18. Siku yaja ambapo Mwenyezi-Mungu atawanyanganya wanawake wa Yerusalemu vitu vyote wanavyoringia: Njuga, kaya, mikufu,
19. vipuli, vikuku, shungi,
20. vitambaa vya kichwani, bangili, vibwebwe, vibweta vya marashi, hirizi,
21. pete, hazama,