Isaya 28:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ole wenye majivuno na walevi wa Efraimu,fahari yake inatoweka kama ua linalonyauka!Naam, fahari iliyotawala bondeni kwenye rutubarutuba;na vichwani kwao walio watu walevi kupindukia!

2. Bwana amejichagulia mtu wake shujaa na mwenye nguvu,ambaye ni kama mvua ya mawe na dhoruba kali,kama tufani ya mafuriko makubwa;kwa mkono wake atawatupa chini ardhini.

3. Majivuno na fahari ya walevi wa Efraimuyatakanyagwakanyagwa ardhini,

4. fahari yake inatoweka kama ua linalonyauka;fahari iliyotawala bondeni kwenye rutubaitakuwa kama tini za mwanzo kabla ya kiangazi;mtu akiziona huzichuma na kuzila mara moja.

Isaya 28