Isaya 25:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe Mungu wangu;nitakutukuza na kulisifu jina lako,kwa maana umetenda mambo ya ajabu;waitekeleza kwa uaminifu na kwelimipango uliyoipanga tangu zamani.

2. Umeufanya mji ule kuwa rundo la mawe,mji wenye ngome kuwa uharibifu.Majumba ya watu wageni yametoweka,wala hayatajengwa tena upya.

3. Kwa hiyo watu wenye nguvu watakutukuza,miji ya mataifa katili itakuogopa.

4. Maana wewe umekuwa ngome kwa maskini,ngome kwa fukara katika taabu zao.Wewe ni kimbilio wakati wa tufani,kivuli wakati wa joto kali.Kweli pigo la watu wakatili ni kalikama tufani inayopiga ukuta;

Isaya 25