Isaya 22:19-23 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Mwenyezi-Mungu atakungoa madarakani mwako na kukuporomosha kutoka mahali ulipo.

20. “Siku hiyo, nitamleta mtumishi wangu Eliakimu mwana wa Hilkia.

21. Nitamvisha vazi lako rasmi, nitamfunga mshipi wako na kumpa madaraka yako. Yeye atakuwa baba kwa watu wa Yerusalemu na kwa ukoo wa Yuda.

22. Nitamwekea begani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Akifungua, hakuna atakayeweza kufunga na akifunga, hakuna atakayeweza kufungua.

23. Nitamwimarisha Eliakimu kama kigingi kilichofungiwa mahali salama, naye atapata heshima tukufu katika ukoo wa wazee wake.

Isaya 22