Isaya 2:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,hazina yao ni kubwa kupindukia.Nchi yao imejaa farasi,magari yao ya kukokotwa hayana idadi.

8. Nchi yao imejaa vinyago vya miungu,huabudu kazi ya mikono yao,vitu walivyotengeneza wao wenyewe.

9. Kwa hiyo, kila mtu ataaibishwa na kufedheheshwa.Usiwasamehe hata kidogo, ee Mungu!

10. Ingieni katika mwamba,mkajifiche mavumbini,kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu,mbali na utukufu wa enzi yake.

11. Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa,majivuno ya kila mtu yatavunjwa;na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.

Isaya 2