8. Wavuvi watalia na kuomboleza,wote watumiao ndoana watalalama;wote wanaotanda nyavu majini watakufa moyo.
9. Wafuma nguo za kitani watakata tamaa,wote kwa pamoja watakufa moyo.
10. Wafuma nguo watafedheheshwa,na vibarua watahuzunika.
11. Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa,washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga!Awezaje kila mmoja kumwambia Farao,“Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi;mzawa wa wafalme wa hapo kale!”
12. Wako wapi, ewe Farao, wataalamu wako?Waache basi wakuambie na kukujulishaaliyopanga Mwenyezi-Mungu wa majeshi dhidi ya Misri!
13. Lakini viongozi wa Soani ni wapumbavu,wakuu wa Memfisi wamedanganyika.Hao walio msingi wa makabila yaowamelipotosha taifa la Misri.
14. Mwenyezi-Mungu amewamwagia hali ya vurugu,wakawapotosha Wamisri katika mipango yao yote,wakawa kama mlevi anayeyumbayumba akitapika.