11. Hivyo, nafsi yangu yalilia Moabu kama kinubi,na moyo wangu kwa ajili ya mji wa Kir-heresi.
12. Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao,wanapojichosha huko juu mahali pa ibada,wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali,hawatakubaliwa.
13. Hili ndilo jambo alilosema Mwenyezi-Mungu wakati uliopita kuhusu Moabu.
14. Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”