10. Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba.Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena,wala kupiga vigelegele.Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni,sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.
11. Hivyo, nafsi yangu yalilia Moabu kama kinubi,na moyo wangu kwa ajili ya mji wa Kir-heresi.
12. Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao,wanapojichosha huko juu mahali pa ibada,wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali,hawatakubaliwa.
13. Hili ndilo jambo alilosema Mwenyezi-Mungu wakati uliopita kuhusu Moabu.
14. Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”