Isaya 11:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,tawi litachipua mizizini mwake.

2. Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,roho ya hekima na maarifa,roho ya shauri jema na nguvu,roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.

3. Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.

4. Atawapatia haki watu maskini,atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.Kwa neno lake ataiadhibu dunia,kwa tamko lake atawaua waovu.

Isaya 11