12. Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi,wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu.
13. Wanapenda kutoa tambiko,na kula nyama yake;lakini mimi Mwenyezi-Mungu sipendezwi hata kidogo.Mimi nayakumbuka makosa yao;nitawaadhibu kwa dhambi zao;nitawarudisha utumwani Misri.
14. Waisraeli wamemsahau Muumba wao,wakajijengea majumba ya fahari;watu wa Yuda wamejiongezea miji ya ngome,lakini mimi nitaipelekea moto miji hiyo,na kuziteketeza ngome zao.”