Hosea 4:2-13 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Kuapa, uongo, mauaji, wizi na uzinzi huzuka humo.Umwagaji damu hufuatana mfululizo.

3. Kwa hiyo, nchi yote ni kame,wakazi wake wote wanaangamiapamoja na wanyama wa porini na ndege;hata samaki wa baharini wanaangamizwa.

4. “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe;maana mimi nakushutumu wewe kuhani.

5. Wewe utajikwaa mchana,naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku.Nitamwangamiza mama yako Israeli.

6. Watu wangu wameangamia kwa kutonijua,maana wewe kuhani umekataa mafundisho.Nimekukataa kuwa kuhani wangu.Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako,nami pia nitawasahau watoto wako.

7. “Kadiri makuhani walivyoongezeka,ndivyo wote walivyozidi kuniasi.Basi, nitaigeuza fahari yao kuwa aibu.

8. Wanajishibisha kwa sadaka za watu wangu wenye dhambi.Wana hamu sana ya kuwaona wametenda dhambi.

9. Lakini yatakayowapata watu yatawapata makuhani;nitawaadhibu kwa sababu ya mwenendo wao,nitawalipiza matendo yao wenyewe.

10. Watakula, lakini hawatashiba;watazini, lakini hawatapata watoto,kwa sababu wameniacha mimi Mwenyezi-Mungu,na kufuata miungu mingine.

11. “Divai mpya na ya zamanihuondoa maarifa.

12. Watu wangu huomba shauri kutoka kwa mti;kijiti chao cha ramli ndicho kinachowapa kauli.Nia ya kufanya uzinzi imewapotosha;wamefanya uzinzi kwa kufuata miungu mingine,wakaniacha mimi Mungu wao.

13. Wanatambikia kwenye vilele vya milima;naam, wanatoa tambiko vilimani,chini ya mialoni, migude na mikwaju,maana kivuli chao ni kizuri.“Kwa hiyo binti zenu hufanya uzinzi,na bibiarusi wenu hufanya uasherati.

Hosea 4