Hosea 4:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Msikilizeni Mwenyezi-Mungu,enyi Waisraeli.Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii.“Hamna tena uaminifu wala wema nchini;hamna anayemjua Mungu katika nchi hii.

2. Kuapa, uongo, mauaji, wizi na uzinzi huzuka humo.Umwagaji damu hufuatana mfululizo.

3. Kwa hiyo, nchi yote ni kame,wakazi wake wote wanaangamiapamoja na wanyama wa porini na ndege;hata samaki wa baharini wanaangamizwa.

4. “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe;maana mimi nakushutumu wewe kuhani.

5. Wewe utajikwaa mchana,naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku.Nitamwangamiza mama yako Israeli.

6. Watu wangu wameangamia kwa kutonijua,maana wewe kuhani umekataa mafundisho.Nimekukataa kuwa kuhani wangu.Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako,nami pia nitawasahau watoto wako.

7. “Kadiri makuhani walivyoongezeka,ndivyo wote walivyozidi kuniasi.Basi, nitaigeuza fahari yao kuwa aibu.

Hosea 4