1. Waefraimu waliponena, watu walitetemeka;Waefraimu walikuwa na uwezo mkubwa huko Israeli,lakini walianza kumwabudu Baali, wakajiletea kifo.
2. Waefraimu wameendelea kutenda dhambi,wakajitengenezea sanamu za kusubu,sanamu zilizotengenezwa kwa ustadi wao,zote zikiwa kazi ya mafundi.Wanasema, “Haya zitambikieni!”Wanaume wanabusu ndama!
3. Basi, watatoweka kama ukungu wa asubuhi,kama umande utowekao upesi;kama makapi yanayopeperushwa mahali pa kupuria,kama moshi unaotoka katika bomba.
4. Mwenyezi-Mungu asema:“Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu,ambaye niliwatoa nchini Misri;hamna mungu mwingine ila mimi,wala hakuna awezaye kuwaokoeni.
5. Ni mimi niliyewatunza mlipokuwa jangwani,katika nchi iliyokuwa ya ukame.
6. Lakini mlipokwisha kula na kushiba,mlianza kuwa na kiburi, mpaka mkanisahau.