1. “Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,Kutoka Misri nilimwita mwanangu.
2. Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita,ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami;waliendelea kuyatambikia Mabaali,na kuvifukizia ubani vinyago vya miungu.
3. Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea!Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu;lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.
4. Niliwaongoza kwa kamba za hurumanaam, kwa kamba za upendo;kama baba amwinuaye mtoto mpaka shavuni mwake,ndivyo nami nilivyokuwa kwao.Mimi niliinama chini na kuwalisha.
5. Basi, watarudi nchini Misri;watatawaliwa na mfalme wa Ashuru,kwa sababu wamekataa kunirudia.
6. “Upanga utavuma katika miji yao,utavunjavunja miimo ya malango yakena kuwaangamiza katika ngome zao.
7. Watu wangu wamepania kuniacha mimi,wakiitwa waje juu,hakuna hata mmoja anayeweza.
8. Ewe Efraimu, nawezaje kukuacha?Nawezaje kukutupa ewe Israeli?Nitawezaje kukufanya kama mji wa Adma?Nitawezaje kukutenda kama Seboimu!Nazuiwa na moyo wangu;huruma yangu imezidi kuwa motomoto.