27. Hizo ndizo koo za Zebuluni, jumla wanaume 60,500.
28. Kabila la Yosefu baba yao Manase na Efraimu.
29. Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi.
30. Yezeri, Heleki,
31. Asrieli, Shekemu,
32. Shemida na Heferi.
33. Selofehadi, mwana wa Heferi hakupata watoto wa kiume bali wa kike tu, nao ni Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirza.
34. Hizo ndizo koo za Manase, jumla wanaume 52,700.
35. Kabila la Efraimu lilikuwa na jamaa za Shuthela, Bekeri na Tahani.