Hesabu 21:13-21 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kutoka huko walisafiri, wakapiga kambi kaskazini ya mto Arnoni, ambao hutiririka kutoka katika nchi ya Waamori na kupitia jangwani. Mto Arnoni ulikuwa mpaka kati ya Wamoabu na Waamori.

14. Kwa sababu hiyo, imeandikwa katika kitabu cha vita vya Mwenyezi-Mungu:“Mji wa Wahebu nchini Sufa,na mabonde ya Arnoni,

15. na mteremko wa mabondeunaofika hadi mji wa Ari,na kuelekea mpakani mwa Moabu!”

16. Kutoka huko Waisraeli walisafiri mpaka Beeri; yaani kisima ambapo Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Wakusanyeni watu pamoja, nami nitawapa maji.”

17. Hapo Waisraeli waliimba wimbo huu:“Bubujika maji ee kisima! – Kiimbieni!

18. Kisima kilichochimbwa na wakuukilichochimbwa sana na wenye cheo,kwa fimbo zao za enzi na bakora.”Kutoka jangwani walisafiri mpaka Matana,

19. kutoka Matana mpaka Nahalieli, kutoka Nahalieli mpaka Bamothi,

20. na kutoka Bamothi mpaka kwenye bonde linaloingia nchi ya Moabu, kwenye kilele cha Mlima Pisga, kielekeacho chini jangwani.

21. Waisraeli walimpelekea mfalme Sihoni wa Waamori, ujumbe huu:

Hesabu 21