Hesabu 17:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mose akaziweka fimbo hizo zote mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano.

8. Kesho yake asubuhi, Mose alikwenda katika hema la mkutano. Humo, aliikuta fimbo ya Aroni wa kabila la Lawi, imechipua na kutoa vichipukizi vilivyochanua maua na kuzaa matunda mabivu ya mlozi.

9. Kisha Mose akazitoa fimbo zote hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akawaonesha Waisraeli wote, na kila kiongozi akachukua fimbo yake.

10. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Irudishe fimbo ya Aroni mbele ya sanduku la agano. Hiyo itatunzwa mahali hapo, na ni onyo kwa waasi hao kwamba wasipoacha kuninungunikia, watakufa.”

11. Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.

12. Waisraeli wakamwambia Mose, “Angalia sasa! Tunaangamia! Tumekwisha! Sote tumekwisha.

13. Kila mtu atakayekaribia, hema la Mwenyezi-Mungu atakufa. Je, tutaangamia sote?”

Hesabu 17