Hesabu 13:9-21 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu.

10. Kabila la Zebuluni, Gadieli mwana wa Sodi.

11. Kabila la Yosefu (yaani kabila la Manase), Gadi mwana wa Susi.

12. Kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali.

13. Kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli.

14. Kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi.

15. Kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.

16. Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani. Mose alimpa Hoshea mwana wa Nuni jina jipya, akamwita Yoshua.

17. Alipowatuma kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani, Mose aliwaambia: “Nendeni juu kule Negebu, hadi kwenye nchi ya milima,

18. mkaipeleleze nchi ilivyo. Chunguzeni pia kama watu wanaoishi humo ni wenye nguvu au dhaifu, wengi au wachache.

19. Pelelezeni kama nchi hiyo ni nzuri au mbaya, na kama miji wanamoishi ni kambi au ni nyumba zilizozungukwa na ngome.

20. Chunguzeni pia kama nchi yenyewe ni tajiri au maskini, ina miti au haina. Muwe na mioyo ya ujasiri na mnaporudi chukueni baadhi ya matunda ya nchi hiyo.” Hayo yalikuwa majira ya zabibu zianzapo kuiva.

21. Basi, watu hao wakaenda na kuipeleleza nchi toka jangwa la Sini hadi Rehobu, karibu na njia ya kuingilia Hamathi.

Hesabu 13