Habakuki 2:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)

18. “Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu?Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa,ni kitu cha kueneza udanganyifu!Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe,kinyago ambacho hakiwezi hata kusema!

19. Ole wake mtu aliambiaye gogo: ‘Amka!’Au jiwe bubu ‘Inuka!’Je, sanamu yaweza kumfundisha mtu?Tazama imepakwa dhahabu na fedha,lakini haina uhai wowote.”

20. Lakini Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu;dunia yote na ikae kimya mbele yake.

Habakuki 2