Ezekieli 17:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Wewe mtu! Tega kitendawili, uwaambie fumbo Waisraeli.

3. Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Kulikuwa na tai mmoja mkubwa sanaaliyekuwa na mabawa makubwa,yenye manyoya marefu mengiyenye rangi za kila aina.Tai huyo aliruka mpaka mlimani Lebanoni,akatua juu ya kilele cha mwerezi;

4. akakwanyua tawi lake la juu zaidi,akalipeleka katika nchi ya wafanyabiashara,akaliweka katika mji wao mmoja.

Ezekieli 17