8. Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine,wapate maji, lakini hayakuwatosha.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
9. “Niliwapiga pigo la ukame na ukungu;nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu;nzige wakala mitini na mizeituni yenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
10. “Niliwaleteeni ugonjwa wa taunikama ule nilioupelekea Misri.Niliwaua vijana wenu vitani,nikawachukua farasi wenu wa vita.Maiti zilijaa katika kambi zenu,uvundo wake ukajaa katika pua zenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
11. “Niliwaangusha baadhi yenu kwa maangamizikama nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.Wale walionusurika miongoni mwenu,walikuwa kama kijiti kilichookolewa motoni.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
12. “Kwa hiyo, enyi Waisraeli, nitawaadhibu.Na kwa kuwa nitafanya jambo hilo,kaeni tayari kuikabili hukumu yangu!”
13. Mungu ndiye aliyeifanya milima,na kuumba upepo;ndiye amjulishaye mwanadamu mawazo yake;ndiye ageuzaye mchana kuwa usiku,na kukanyaga vilele vya dunia.Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lake!