11. Niliwateua baadhi ya wana wenu wawe manabii,na baadhi ya vijana wenu wawe wanadhiri.Je, enyi Waisraeli,haya nisemayo si ya kweli?Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
12. Lakini nyinyi mliwafanya wanadhiri wanywe divai,na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.
13. “Sasa basi, nitawagandamiza mpaka chini,kama gari lililojaa nafaka.
14. Hata wapiga mbio hodari hawataweza kutoroka;wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,na askari watashindwa kuyaokoa maisha yao.
15. Wapiga upinde vitani hawatastahimili;wapiga mbio hodari hawataweza kujiokoa,wala wapandafarasi hawatayanusurisha maisha yao.
16. Siku hiyo, hata askari hodariwatatimua mbio bila chochote.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”