1. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomukwa kuichoma moto mifupa yakeili kujitengenezea chokaa!
2. Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu,na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi.Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta,watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.
3. Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu,pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
4. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamepuuza sheria zangu,wala hawakufuata amri zangu.Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.
5. Basi, nitaishushia moto nchi ya Yuda,na kuziteketeza kabisa ngome za Yerusalemu.”