Amosi 1:2-6 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Amosi alisema hivi:Mwenyezi-Mungu ananguruma kutoka mlima Siyoni,anavumisha sauti yake kutoka Yerusalemu,hata malisho ya wachungaji yanakauka,nyasi mlimani Karmeli zinanyauka.

3. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Damasko wametenda dhambi tena na tena;kwa hiyo, sitaacha kuwaadhibu;waliwatendea watu wa Gileadi ukatili mbaya.

4. Basi, nitaishushia moto ikulu ya mfalme Hazaeli,nao utaziteketeza kabisa ngome za mfalme Ben-hadadi.

5. Nitayavunjavunja malango ya mji wa Damasko,na kuwang'oa wakazi wa bonde la Aweni,pamoja na mtawala wa Beth-edeni.Watu wa Aramu watapelekwa uhamishoni Kiri.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

6. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka watu kabila zima,wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.

Amosi 1