2 Wakorintho 7:13-16 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Ndiyo maana sisi tulifarijika sana.Siyo kwamba tulifarijika tu, ila pia Tito alitufurahisha kwa furaha aliyokuwa nayo kutokana na jinsi mlivyomchangamsha moyo.

14. Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia nyinyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli tupu.

15. Hivyo upendo wake wa moyo kwenu nyinyi unaongezeka zaidi akikumbuka jinsi nyinyi nyote mlivyo tayari kutii, na jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu nyingi na kutetemeka.

16. Nafurahi sana kwamba naweza kuwategemea nyinyi kabisa katika kila jambo.

2 Wakorintho 7