2 Mambo Ya Nyakati 32:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Baada ya mambo yote hayo ya uaminifu ya mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliivamia Yuda. Alikuja akapiga makambi kwenye miji yenye ngome akitumaini kwamba ataishinda iwe mali yake.

2. Mfalme Hezekia alipoona kwamba mfalme Senakeribu amekuja kwa kusudi la kuishambulia Yerusalemu,

3. aliamua, yeye pamoja na maofisa wake wakuu wa majeshi kuyafunga maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya miji; nao wakamuunga mkono, wakamsaidia.

4. Wakawakusanya watu wengi pamoja wakazifunga chemchemi zote pamoja na kijito kilichopitia kati ya sehemu hiyo wakisema, “Ya nini kuwaachia wafalme wa Ashuru wakija wakute maji tele?”

2 Mambo Ya Nyakati 32