13. Meshulamu alimzaa Hilkia, Hilkia alimzaa Azaria,
14. Azaria alimzaa Seraya, Seraya alimzaa Yehosadaki;
15. Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.
16. Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari.
17. Kila mmoja wao pia alikuwa na wana. Gershomu aliwazaa Libni na Shimei;
18. Kohathi aliwazaa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli;
19. naye Merari aliwazaa Mahli na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kulingana na koo zao.
20. Wafuatao ndio wazawa wa Gershomu kutoka kizazi hadi kizazi: Gershomu alimzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima,