11. Azaria alimzaa Amaria, Amaria alimzaa Ahitubu,
12. Ahitubu alimzaa Sadoki, Sadoki alimzaa Meshulamu,
13. Meshulamu alimzaa Hilkia, Hilkia alimzaa Azaria,
14. Azaria alimzaa Seraya, Seraya alimzaa Yehosadaki;
15. Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.
16. Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari.