12. Eshtoni alikuwa na wana watatu: Beth-rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa mwanzilishi wa mji wa Ir-nahashi. Wazawa wa watu hawa waliishi Reka.
13. Wana wa Kenazi walikuwa: Othnieli na Seraya; na wana wa Othnieli walikuwa Hathathi na Meonothai.
14. Meonothai alimzaa Ofra. Seraya alimzaa Yoabu, mwanzilishi wa Bonde la Mafundi, lililopewa jina hilo kwa sababu wote waliokuwa humo walikuwa mafundi stadi.
15. Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu: Iru, Ela na Naamu. Na mwana wa Ela alikuwa Kenazi.
16. Wana wa Yehaleli walikuwa Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.
17. Wana wa Ezra walikuwa Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Meredi alimwoa Bithia, bintiye Farao, na hawa ndio wana aliomzalia Meredi: Miriamu, Shamai na Ishba, mwanzilishi wa mji wa Eshtemoa.
18. Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi. Huyu alimzalia Yeredi, mwanzilishi wa Mji wa Gedori, Heberi, mwanzilishi wa mji wa Soko, na Yekuthieli, mwanzilishi wa Mji wa Zanoa.
19. Hodia alimwoa dada yake Nahamu ambaye wazawa wake ndio waanzilishi wa kabila la Garmi, lililoishi katika mji wa Keila, na kabila la Maakathi, lililoishi katika mji wa Eshtemoa.
20. Wana wa Shimoni walikuwa Amnoni, Rina, Ben-hanani na Tiloni. Ishi alikuwa na wana wawili: Zohethi na Ben-zohethi.