1 Mambo Ya Nyakati 2:43-48 Biblia Habari Njema (BHN)

43. Hebroni alikuwa na wana wanne: Kora, Tapua, Rekemu na Shema.

44. Shema alikuwa baba yake Rahamu na babu yake Rekemu. Rekemu nduguye Shema alimzaa Shamai,

45. Shamai akamzaa Maoni, na Maoni akamzaa Beth-suri.

46. Kalebu alikuwa na suria, jina lake Efa. Huyu alimzalia wana wengine watatu: Harani, Mosa na Gazezi. Harani alimzaa Gazezi.

47. Yadai alikuwa na wana sita: Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.

48. Kalebu alikuwa na suria mwingine jina lake Maaka. Huyu alimzalia wana wawili: Sheberi na Tirhana.

1 Mambo Ya Nyakati 2