28. Wana wa Onamu walikuwa Shamai na Yada. Nao wana wa Shamai walikuwa Nadabu na Abishuri.
29. Abishuri alioa mke, jina lake Abihaili, naye akamzalia wana wawili: Abani na Molidi.
30. Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu; lakini Seledi alifariki bila watoto.
31. Apaimu alikuwa na mwana mmoja aliyeitwa Ishi. Ishi alimzaa Sheshani, na Sheshani akamzaa Alai.
32. Yada, nduguye Shamai, alikuwa na wana wawili: Yetheri na Yonathani. Lakini Yetheri alifariki bila watoto.
33. Yonathani alikuwa na wana wawili: Pelethi na Zaza. Wote hao ni wazawa wa Yerameeli.
34. Sheshani hakuwa na watoto wa kiume; alikuwa na binti tu. Hata hivyo, alikuwa na mtumwa wa Kimisri, jina lake Yarha.