7. Basi, hiyo ikawa siku ambayo kwa mara ya kwanza, Daudi alimpa Asafu na ndugu zake Walawi wajibu wa kumwimbia Mwenyezi-Mungu nyimbo za shukrani.
8. Mpeni shukrani Mwenyezi-Mungu,tangazeni ukuu wake,yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda!
9. Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa;simulieni matendo yake ya ajabu!
10. Jisifieni jina lake takatifu;wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi.
11. Mwendeeni Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu;mwendeeni Mwenyezi-Mungu daima.
12. Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda,maajabu yake na hukumu alizotoa,
13. enyi wazawa wa Abrahamu, mtumishi wake,enyi wazawa wa Yakobo, wateule wake.
14. Yeye Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu;hukumu zake zina nguvu duniani kote.
15. Yeye hulishika agano lake milele,hutimiza ahadi zake kwa vizazi elfu.