7. Basi, hiyo ikawa siku ambayo kwa mara ya kwanza, Daudi alimpa Asafu na ndugu zake Walawi wajibu wa kumwimbia Mwenyezi-Mungu nyimbo za shukrani.
8. Mpeni shukrani Mwenyezi-Mungu,tangazeni ukuu wake,yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda!
9. Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa;simulieni matendo yake ya ajabu!
10. Jisifieni jina lake takatifu;wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi.
11. Mwendeeni Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu;mwendeeni Mwenyezi-Mungu daima.