4. Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu;Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili;Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.
5. Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;Sujuduni penye kiti cha miguu yake;Ndiye mtakatifu.
6. Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake,Walipomwita Bwana aliwaitikia;
7. Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao.Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.
8. Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusameheIngawa uliwapatiliza matendo yao.