Zab. 91:3-7 Swahili Union Version (SUV)

3. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.

4. Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5. Hutaogopa hofu ya usiku,Wala mshale urukao mchana,

6. Wala tauni ipitayo gizani,Wala uele uharibuo adhuhuri,

7. Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume!Hata hivyo hautakukaribia wewe.

Zab. 91