2. Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini.
3. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.
4. Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5. Hutaogopa hofu ya usiku,Wala mshale urukao mchana,
6. Wala tauni ipitayo gizani,Wala uele uharibuo adhuhuri,