Zab. 88:4-7 Swahili Union Version (SUV)

4. Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni;Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.

5. Miongoni mwao waliokufa nimetupwa,Kama waliouawa walalao makaburini.Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,Wametengwa mbali na mkono wako.

6. Mimi umenilaza katika shimo la chini,Katika mahali penye giza vilindini.

7. Ghadhabu yako imenilemea,Umenitesa kwa mawimbi yako yote.

Zab. 88