Zab. 87:3-6 Swahili Union Version (SUV)

3. Umetajwa kwa mambo matukufu,Ee Mji wa Mungu.

4. Nitataja Rahabu na BabeliMiongoni mwao wanaonijua.Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;Huyu alizaliwa humo.

5. Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,Huyu na huyu alizaliwa humo.Na Yeye Aliye juuAtaufanya imara.

6. BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,Huyu alizaliwa humo.

Zab. 87