Zab. 86:7-16 Swahili Union Version (SUV)

7. Siku ya mateso yangu nitakuita,Kwa maana utaniitikia.

8. Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,Wala matendo mfano wa matendo yako.

9. Mataifa yote uliowafanya watakuja;Watakusujudia Wewe, Bwana,Watalitukuza jina lako;

10. Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,Wewe ndiwe mfanya miujiza,Ndiwe Mungu peke yako.

11. Ee BWANA, unifundishe njia yako;Nitakwenda katika kweli yako;Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;

12. Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu,Kwa moyo wangu wote,Nitalitukuza jina lako milele.

13. Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana;Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

14. Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia;Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho.Wala hawakukuweka WeweMbele ya macho yao.

15. Lakini Wewe, Bwana,U Mungu wa rehema na neema,Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.

16. Unielekee na kunifadhili mimi;Mpe mtumishi wako nguvu zako,Umwokoe mwana wa mjakazi wako.

Zab. 86