Zab. 84:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Maskani zako zapendeza kama nini,Ee BWANA wa majeshi!

2. Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA,Naam, na kuzikondea.Moyo wangu na mwili wanguVinamlilia Mungu aliye hai.

3. Shomoro naye ameona nyumba,Na mbayuwayu amejipatia kioto,Alipoweka makinda yake,Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi,Mfalme wangu na Mungu wangu.

4. Heri wakaao nyumbani mwako,Wanakuhimidi daima.

5. Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.

Zab. 84