Zab. 83:14-17 Swahili Union Version (SUV)

14. Kama moto uteketezao msitu,Kama miali ya moto iiwashayo milima,

15. Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako,Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

16. Uwajaze nyuso zao fedheha;Wakalitafute jina lako, BWANA.

17. Waaibike, wafadhaike milele,Naam, watahayarike na kupotea.

Zab. 83