Zab. 78:22-32 Swahili Union Version (SUV)

22. Kwa kuwa hawakumwamini Mungu,Wala hawakuutumainia wokovu wake.

23. Lakini aliyaamuru mawingu juu;Akaifungua milango ya mbinguni;

24. Akawanyeshea mana ili wale;Akawapa nafaka ya mbinguni.

25. Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.

26. Aliuelekeza upepo wa mashariki mbinguni;Akaiongoza kusi kwa uweza wake.

27. Akawanyeshea nyama kama mavumbi,Na ndege wenye mbawa,Kama mchanga wa bahari.

28. Akawaangusha kati ya matuo yao,Pande zote za maskani zao.

29. Wakala wakashiba sana;Maana aliwaletea walivyovitamani;

30. Hawakuachana na matakwa yao.Ila chakula chao kikali ki vinywani mwao

31. Hasira ya Mungu ikapanda juu yao,Akawaua waliokuwa wanono;Akawaangusha chini vijana wa Israeli.

32. Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi,Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.

Zab. 78