Zab. 72:5-13 Swahili Union Version (SUV)

5. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua,Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi.

6. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa,Kama manyunyu yainyweshayo nchi.

7. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.

8. Na awe na enzi toka bahari hata bahari,Toka Mto hata miisho ya dunia.

9. Wakaao jangwani na wainame mbele zake;Adui zake na warambe mavumbi.

10. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi;Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.

11. Naam, wafalme wote na wamsujudie;Na mataifa yote wamtumikie.

12. Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo,Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.

13. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,Na nafsi za wahitaji ataziokoa.

Zab. 72