Zab. 69:24-27 Swahili Union Version (SUV)

24. Uimwage ghadhabu yako juu yao,Na ukali wa hasira yako uwapate.

25. Matuo yao na yawe ukiwa,Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.

26. Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe,Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha.

27. Uwaongezee uovu juu ya uovu,Wala wasiingie katika haki yako.

Zab. 69